Matukio mbalimbali 2019 (2)
Sekondari ya Eagles imeanzisha tahsusi mpya za PMCs, PCsG, na CBCs zenye somo jipya la Computer Science.
Wanafunzi wa kidato cha tano wakiwa darasani wakifuatilia somo la Computer Science kwenye Projector. Sekondari ya Eagles imeanzisha tahsusi mpya za PMCs, PCsG, na CBCs zenye somo jipya la Computer Science.
Eagles High School yapata matokeo mazuri ya mtihani wa Form 6 (ACSEE 2019)
Uongozi wa shule ya Eagles Hiugh School unayo furaha kuwatangazia kuwa umepokea matokeo mazuri ya mtihani wa Form 6 (ACSEE 2019).
DIVISION I 16
DIVISION II 56
DIVISION III 36
DIVISION IV 1
JUMLA 109
Wanaojiunga kidato cha tano 2019
Wanafunzi wetu 63 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2018 wamepata post mbalimbali kwenda kidato cha tano na vyuo mbalimbali vya serikali. Mchanganuo wa waliochaguliwa ni kama ifuatavyo: HGL- 11, PCM-9, PCB-1, HGE-8, PGM-2, HKL-2, EGM-6, ECA-7
Hali kadhalika wanafunzi wa Sekondari ya Eagles waliochaguliwa kwenda vyuo mbalimbali kwa stashahada na astashahada ni 17.
Tunatoa pongezi sana kwa wazazi na walimu kwa juhudi na ushirikiano mzuri waliounesha hadi kufikia mafanikio haya.
Timu ya sekondari ya Eagles yashiriki kwa mafanikio makubwa kwenye Michezo ya Umiseta ngazi ya wilaya, 25/Mei/2019
Kwa mara nyingine wanafunzi wa sekondari ya Eagles wamethibitisha uhodari wao sio tu katika masomo peke yake, bali pia hata katika Michezo ya Umiseta ngazi ya wilaya iliyofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25/Mei/2019.
Mara hii michezo hii ngazi ya wilaya ilifanyika katika Shule ya sekondari Bagamoyo. Wanafunzi wengi wa sekondari ya Eagles walichaguliwa kushiriki michezo ya Umiseta ngazi ya mkoa itakayofanyika Kibaha.
Kwenye michezo hiyo wanafunzi wa sekondari ya Eagles waliambatana na mratibu wa michezo Mwl. Sharif Mgulla ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuanda timu hiyo. Kwenye mojawapo ya picha hapa chini ni mtu wa tatu kutoka kushoto aliyevalia t-shirt ya blue.
Matukio mbalimbali 2019
Picha mbalimbali za matukio ya mahafali ya kidato cha sita 2019 yaliyofanyika tarehe 06.05.2019 shuleni Eagles. Waliovalia fulana ni wahitimu wa kidato sita wakifurahia siku hii muhimu.
Meneja wa Sekondari ya Eagles Bw George Fumbuka akizungumza na wahitimu siku ya mahafali ya Form VI 2019
Graduation ceremony for form VI students 2019
Various pictures from the recent graduation ceremony for form VI students 2019, which took place at Eagles High School (EHS) on Saturday 6th of May 2019. Students wearing t-shirts are the form-six graduates enjoying this important day.