Eagles ni shule ya sekondari ya wavulana, wote bweni, yenye Kidato cha 1 hadi cha 6. Imesajiliwa kama shule binafsi kwa namba S.2397 mwaka 2006 kutoa elimu ya sekondari kwa mitaala ya Tanzania. Shule yetu iko umbali wa kilometa 2 kutoka kituo kipya cha mabasi cha Bagamoyo karibu na kanisa kongwe Katoliki na Chuo cha ADEM upande wa magharibi.

TAALUMA:

MCHANGANUO WA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2015-2019

MWAKA

DIVISION I

DIVISION II

DIVISION III

DIVISION IV / ZERO

2015

4

5

11

0

2016

11

29

23

0

2017

7

35

54

0

2018

16

40

24

0

2019

16

56

36

0

Shule ina mazingira mazuri ya kitaaluma, walimu wa kutosha wenye sifa na mikakati mizuri ya kitaaluma yenye lengo la kumwezesha mwanafunzi kufaulu masomo yake. Aidha, Shule imeanzisha mfumo wa kufundisha kwa kutumia iPads za Apple zilizounganishwa na mtandao (Internet) ikiwa ni mkakati wa kuboresha ufundishaji ili uendane na teknolojia ya mawasiliano. Shule inayo masomo yote ya Sayansi, Sanaa, Biashara, Kilimo, Lugha na Kompyuta. Kwa Kidato cha 5 na cha 6 shule ina tahsusi zifuatazo:

Sanaa/Lugha: HGL (History, Geography, (English) Language); HGK (History, Geography, Kiswahili), HKL (History, Kiswahili, Language); KLF (Kiswahili, Language, French)

Biashara: ECA (Economics, Commerce, Accountancy); EGM (Economics, Geography, Mathematics); HGE (History, Geography, Economics); AgBE (Agriculture, Biology, Economics)

Sayansi: PCM (Physics, Chemistry, Mathematics); PCB (Physics, Chemistry, Biology); CBG (Physics, Biology, Geography); PMCs (Physics, Mathematics, Computer Science); CBCs (Chemistry, Biology, Computer Science); PCsG (Physics, Computer Science, Geography); PGM (Physics, Geography, Mathematics), CBA (Chemistry, Biology, Agriculture).

NIDHAMU:

Shule inatambua kuwa nidhamu nzuri kwa wanafunzi na watumishi ni muhimu kwa maendeleo ya kitaaluma hivyo imejiwekea mfumo mzuri kusimamia nidhamu. Shule imeweka utaratibu wa kuwa na Walimu walezi wakazi (Resident Parents) kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi baada ya saa za masomo darasani na bwenini. Pia shule ina Mshauri Nasaha (Counselor) kwa lengo la kuwasaidia Wanafunzi (na wazazi wao wakitaka) kitaaluma na kimaadili. Kwa kutambua umuhimu wa dini, shule imeweka utaratibu kila mwanafunzi kuabudu kwa imani yake. Viongozi wa dini hufika shuleni kila siku ya Ijumaa kuongoza shughuli za dini kwa utaratibu wa serikali.

AFYA NA MAZINGIRA:

Shule ina mazingira mazuri na tulivu ya mwanafunzi kujisomea. Mazingira yote ya shule ni safi kwa ustawi wa afya za wanafunzi. Pia shule ina mpangilio mzuri wa chakula ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mlokamili wakiwa shuleni. Shule ina miti ya matunda pamoja na bustani za mbogamboga ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe kamili. Aidha, tunao wauguzi (nurses) wawili kwa ajili ya kuhudumia afya za wanafunzi masaa 24. Wanafunzi wote wameunganishwa na bima ya afya (NHIF), kila mtu na kadi yake, kwa lengo la kurahisisha matibabu.

MICHEZO:

Kila mwanafunzi awapo Shuleni anatakiwa kushiriki katika michezo mbalimbali kwa lengo la kujenga afya ya mwili na akili pamoja na kuimalisha vipaji. Shule ina viwanja vizuri vya michezo ikiwemo mpira wa miguu (football), mpira wa kikapu (basketball) na mpira wa wavu (volleyball). Wapo walimu wa michezo pamoja na kufundisha michezo. Shule ya Sekondari Eagles imekuwa na rekodi nzuri katika michezo na imekuwa ikishiriki vizuri mechi mbalimbali ndani na nje ya shule hadi ngazi ya kitaifa.

ADA ZA SHULE

Ada ya shule ni shilingi 3,300,000/=. Inaweza ikalipwa mara moja au kwa mafungu manne yaani kuanzia shilingi 1,500,000/= unapojiunga halafu shilingi 600,000/= mafungu matatu mwezi Machi, Juni na Septemba. Mwanafunzi atatakiwa aje na mahitaji yake kama godoro, shuka, vitabu, sare za shule (vyote vitaainishwa kwenye Barua ya maelekezo ya kujiunga (Joining Instructions). Tuna utaratibu wa Pre-Form 1 na Pre-Form 5 ambao umeelezwa hapa chini. Malipo yako yatapunguzwa kwenye ada ya shule mwakani.

Shule ina maabara inayojitosheleza kwa masomo ya sayansi na kompyuta; na eneo kubwa kwa shughuli za kilimo.

NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA 2020 KIDATO CHA 1 NA CHA 5:

Udahili wa masomo ya Kidato cha 1 na Kidato cha 5 kwa mwaka 2020 umeanza kwa wanafunzi wanaomaliza Darasa la 7 au Kidato cha 4 mwaka 2019. Kidato cha 1 hufanyiwa mtihani wa majaribio (aptitude test), ikiwa ni pamoja na wahamiaji wote.

Wanafunzi wa Kidato cha 5 hawafanyiwi mtihani wa majaribio, mwanafunzi atatakiwa tu awe na ufaulu wa matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 angalau point 10 (CCD) kwenye tahsusi anayotaka kusoma.

MASOMO YA PRE-FROM 1 NA PRE-FORM 5

Masomo ya awali ya kidato cha 1 (Pre-Form 1) yameanza rasmi tarehe 1 Oktoba 2019 kwa wiki 12 hadi tarehe 14 Disemba 2019. Malipo ni shilingi 450,000/= ambazo zitapunguzwa kwenye ada za shule mwakani.

Masomo ya awali ya Kidato cha Tano (Pre Form 5) yataanza rasmi tarehe 1 Machi 2020 na yataendelea kwa wiki 8. Gharama ya masomo hayo na malazi ni shilingi 300,000/= ambayo nayo itapunguzwa kwenye ada ya kidato cha 5 kwa masomo yatakayoanza mwezi Julai 2020.

MAWASILINO:

Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni, Msimbazi Centre Chumba namba 9 na kwenye tovuti ya shule www.eaglessecondary.com. Kwa mawasiliano tumia mojawapo ya simu hizi zifuatazo: 0738719870 / 0738719875 / 0738719877 / 0769918108 / 0655303759

Simu ya Mkuu wa Shule ofisini ni 0232440282 Bagamoyo

Baruapepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.; This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.. Pia tuko kwenye Twitter, Instagram, Facebook na Pinterest.

 

Gallery: Graduation and inauguration ceremony

Gallery: Library and computer lab